EACC Yawahimiza Wataalamu Na Mashirika Ya Kijamii Kupambana Na Ufisadi

Afisa mkuu wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi-EACC, Halakhe Waqo amewahimiza wataalamu na mashirika la kijamii kusaidia katika juhudi za kupambana na ufisadi. Waqo alisema juhudi za kukabiliana na ufisadi haziwezi kufanikiwa pasipo juhudi za pamoja. Afisa huyo alisema vita dhidi ya ufisadi sio jukumu la serikali pekee, bali la wakenya walio na nia njema. Akiongea alipowahutubia wanachama wa taasisi ya mahasibu hapa nchini wakati wa kikao cha kila mwezi kuhusu uongozi, Waqo aliwataja mahasibu na mawakili kuwa muhimu katika kukabiliana na uovu huo. Wakati uo huo, Waqo alitoa wito kwa wananchi wawe na subira ili kuiwezesha tume hiyo kufanya uchunguzi unaofaa. Alisema uchunguzi sharti ufanywe kwa kuzingatia kanuni zilizowekwaa