EACC Yasema Gavana Wa Murang’a Ana Kesi Ya Kujibu

Tume ya kukabiliana na ufisadi nchini imesema gavana wa Muranga  Mwangi wa Iria ana kesi ya kujibu kufuatia kutiwa nguvuni kwake  katika mtaa wa Parklands hapa Nairobi.Tume hiyo ilisema  Wa Iria atashtakiwa kwa kuwatatiza makachero waliokuwa wakiendesha shughuli zao rasmi.Madai hayo yalitokea nyumbani kwa  Wa Iria huko Murang’a mwezi januari mwaka huu wakati maafisa wa tume hiyo walipokuwa wakitekeleza agizo la mahakama la kusaka nyumba yake.Afisa wa mawasiliano wa tume hiyo Yassin Aila Amaro alidhibitisha kutiwa nguvuni mwa kiongozi huyo akiongeza kuwa gavana huyo atafikishwa mahakamani hii leo.