EACC kukagua maisha ya wafanyikazi wa serikali kaunti ya Taita Taveta

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi itazindua ukaguzi wa mtindo wa maisha kwa wafanyakazi wote wa serikali ya kaunti ya Taita Taveta ili kubainisha jinsi walivyopata utajiri wao muda mfupi baada ya kuajiriwa. Tume hiyo imezindua rasmi shughuli ya wiki mbili ya kutathmini hatari ya ufisadi katika kaunti hiyo ili kubainisha iwapo kumekuwa na ukosefu wa maadili A�katika usimamizi wa pesa za umma. Wakati wa ziara yake katika afisi ya gavana wa kaunti hiyo A�Granton Samboja, naibu mwenyekiti wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC Sophia Lepuchirit alisema wengi wa wafanyakazi wa kaunti hiyo wamejipatia mamilioni ya pesa kwa A�muda mfupi mno . Lepuchirit alisema tume hiyo itaharakisha kuchunguza kila mfanyakazi katika kaunti hiyo na kusema ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali ilipata na hatia kaunti nyingi hasa kuhusu swala la pesa za umma. Alisema tume hiyo itachunguza mali ambayo wafanyakazi wanamiliki ikilinganishwa na mishahara yao na kuchunguza iwapo inawezekana kwa mtu kumiliki malori mengi na nyumba kwa kutumia mishahara wanayolipwa. Gavana A�Samboja ameunga mkono matamshi ya kamishna huyo akisema kaunti hiyo imepoteza mamilioni ya pesa kupitia maafisa walaghai wa uikusanyaji ushuru. Alisema serikali yake itashirikiana na wadau wengine kubuni mbinu makhsusi za kukabiliana na ufisadi.