Duale Asema Hababaishwi Na Vitisho Vya CORD Kumpeleka ICC

Kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa,Aden Duale, amesema hababaishwi na vitisho kutoka kwa muungano wa upinzani CORD vya kutoa wito kwa mahakama ya ICC iingilie kati iwapo Jubilee haitamshtaki kwa madai kwamba alitoa matamshi ya chuki ambayo yamesambazwa kupitia mitandao ya kijamii.Akimjibu kiongozi mwenza wa muungano wa CORD kalonzo Musyoka kwamba upinzani unafikiria kumshtaki katika mahakama ya ICC, Duale alisema amekuwa katika mahakama hiyo ya ICC mara kadhaa na kamwe hatatishwa na upinzani.Mbunge huyo wa eneo bunge la Garissa mjini amesema tayari ameandikisha taarifa na idara ya upepelezi akitaka uchunguzi ufanywe kubainisha aliyetoa matamshi hayo ambayo amesema ni ya Uongo.