Duale amshutumu mudavadi kwa kuikosoa serikali kwa kutoza bidhaa za petroli ushuru wa zaidi ya thamani

Kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa, Aden Duale, amemshutumu kiongozi wa chama cha Amani National Congress, Musalia Mudavadi, kwa kuikosoa serikali kwa hatua yake ya kuanza kutoza ushuru wa ziada wa thamani bidhaa za petroli.

Mudavadi amenukuliwa na vyombo vya habari akisema ushuru huo unatokana na ufisadi ambao umekithiri katika sekta ya kawi na ukopaji madeni ya kigeni kiholela.Mudavadi alisema baada ya kuzingatia bei ya mafuta, usafirishaji kwa mabomba na uhifadhi wa mafuta hayo, bei ya lita moja ya petrol inafaa kuwa shillingi 72.61.

Lakini akiongea huko Bura katika kaunty ya Tana River wakati wa mkutano wa hadhara, Duale alisema kiongozi huyo wa chama cha ANC hana idhini ya kuiagiza serikali ya jubilee jinsi inavyofaa kuendesha masuala ya taifa akisema Musalia alikuwa waziri wa fedha wakati serikali ilipopoteza mamilioni ya pesa kupitia kashfa ya Goldernberg.

Duale kwa mara nyingine amelishutumu bunge la senate kwa kushindwa kutekeleza jukumu lake la kuidhinisha miswada kadhaa iliyopitishwa na bunge la kitaifa.