Donald Trump Asema Kuwa Wapinzani Wake Ni Miongoni Mwa Wasomi Wanaotafuta Mbinu Za Kusalia Mamlakani

Waraka wa wazi uliotiwa saini na wataalamu 50 wa maswala ya usalama wa A�chama cha Republican,umesema kuwa ,ikiwa mgombea urais wa chama hicho Donald Trump atachaguliwa kuwa rais huenda akawa rais asiojali kuwahi kuchaguliwa katika historia ya taifa hilo.Watalaamu hao ambao wanajumuisha aliyekuwa mkurugenzi wa A�idara ya ujasusi ya Marekani Michel Hayden walisema kuwa Trump hana staha,maadili na ujuzi wa kuwa rais wa taifa hilo.Wengi wa wale waliotia saini waraka huo,walikuwa wamekataa kuutia saini A�hapo awali mnamo mwezi wa Machi.Akigusia waraka huo ,Truimp alisema kuwa wapinzani wake hao ni miongoni mwa A�wasomi wanaotafuta mbinu za kusalia mamlakani.Haya yanajiri baada ya wafwasi wa ngazi za juu kutoka chama hicho jkukataa kumuidhinisha mkasi huyo atakayewania urais kwa tiketi ya chama cha Republican.Trump alikuwa ameelezea tashwishi yake ikiwa Marekani inapaswa kuendelea kuunga mkono ushirika wa kujihami wa NATO.Aidha alipendekeza kuwa mataifa ya Korea Kusini na Japan yajihami kwa zana za nyuklia.