Donald Trump anuia kumteua John Bolton kuchukuwa mahala pa mshauri wa maswala ya usalama wa kitaifa

Rais A�Donald Trump ananuia kumteuwa aliyekuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa John Bolton kuchukuwa mahala pa mshauri wa maswala ya usalama wa kitaifa nchini humo HR McMaster . Trump aliandika ujumbe katika mtandao wa twitter akimshukuru jenerali A�McMaster, na kusema kuwa alifanya kazi nzuri na daima atasalia kuwa rafiki yake . A�Bolton, ambaye ameunga mkono kushambuliwa kwa Korea Kaskazini na Iran, aliliambia shirika la habari la Fox kwamba jukumu lake litakuwa ni kuhakikisha kuwa rais ana aina mbali mbali za maamuzi . Jenerali McMaster ni mtu maarufu zaidi wa hivi punde kutimuliwa kutoka A�ilikulu ya rais . Bwana Bolton ambaye uteuzi wake hauhitaji kuidhinishwa na bunge la seneti, atakuwa mshauri wa tatu wa rais Trump kuhusiana na maswala ya usalama wa kitaifa katika muda wa miezi 14. Ataanza kutekeleza majukumu yake tarehe 9 mwezi Aprili.