Donald Trump ameahidi kutoa jibizo la nguvu kwa madai ya shambulizi la kemikali

Rais Donald Trump wa marekani ameahidi kutoa jibizo la nguvu kwa madai ya shambulizi la kemikali huko Syria, huku viongozi wa nchi za magharibi wakifikiria hatua watakayochukua. Kulingana na Trump, marekani inafahamu aliyehusika na tukio hilo huko Douma. Duru za huduma za matibabu zilisema watu wengi waliuawa katika shambulizi hilo lakini idadi kamili haijulikani. Pia Trump alijadili kuhusu tukio hilo na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na viongozi wote wawili wakaelezea azma yao ya kuchukua hatua. Hapo mwezi Februari Macron alitisha kuishambulia Syria ikiwa itabainika kuwa ilitumia silaha za kemikali. Kwa upande wake Waziri mkuu wa uingereza Theresa May alishutumu shambulizi hilo la kemikali na akatoa wito kwa wanaomuunga mkono Rais Bashar al-Assad wa Syria wawajibike