Djibouti Yatangaza Kumuunga Mkono Amina Mohamed

Djibouti leo imetangaza kwamba itamuunga mkono waziri wa mashauri ya nchi za kigeni,A�A�Amina Mohamed kuwania uwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Djibouti Mahmoud Ali Youssouf amesema wakati umewadia kwa eneo la Afrika Mashariki kuchukuwa wadhifa huo, akiongeza kuwa baloziA�Amina ndiye anayefaa kushikilia wadhifa huo. Waziri huyo wa Djibouti alisema hayo katika ikulu ya Nairobi alipomkabidhi rais uhuru Kenyatta ujumbe maalum kutoka kwa rais Guelleh. Youssouf pia ni mjumbe maalum wa rais IsmaA?l Omar Guelleh. Rais Kenyatta alishukuru uamuzi huo wa Djibouti akisema balozi Mohamed ni mwaniaji mwenye ujuzi mwingi anayeweza kuiongoza vilivyo tume hiyo ya muungano wa Afrika. Rais alitoa wito kwa mataifa ya Afrika Mashariki kumpigia debe baloziA�Mohamed. RaisA�Kenyatta na waziri huyo wa maswala ya kigeni wa Djibouti pia walijadili hali ilivyo nchini Sudan Kusini na Somalia na kukariri haja ya kutekeleza juhudi mwafaka kudumisha amani na uthabiti katika mataifa hayo mawili.