Derrick a�?Gauchoa�� Onyango Ashukuru kilabu Cha Mathare United na Sony Sugar

Mshambulizi wa Mathare United Derrick a�?Gauchoa�� Onyango ameshukuru kilabu hicho na kile cha Sony Sugar kwa kumwezesha kuboresha mchezo wake.

Chipukizi huyo aliifungia Mathare bao la ushindi dhidi ya Sony Sugar katika mechi ya ligi ya Sportpesa baina ya timu hizo mbili mwishoni mwa juma. Kabla ya kujiunga na a�?slum boysa�? mwezi Januari mwaka huu, Onyango nusura asajiliwe na mojawapo ya Chemilil Sugar au Sony Sugar.

Alihudhuria majaribio ya siku tano katika timu ya Sony kabla ya kujiunga na Mathare United. Onyango amesema ametulia vyema katika kilabu hicho na ligini, huku akitoa shukrani kwa wakufunzi wake, wakiongozwa na kocha Francis Kimanzi.

Awali, chipukizi huyo alikichezea kilabu cha Mbotela Kamaliza kinachoshiriki ligi ya daraja ya chini jijini Nairobi.