Dereva wa trela ambayo ilisababisha ajali atarajiwa kufikishwa mahakamani

Dereva wa trela ambalo lilisababisha ile ajali iliyotokea kwenye barabara kuu kati yaA�A�Narok na Mai Mahiu ambapo abiria 17 walifariki ,anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo.Msemaji wa polisiA�Charles Owino, alisema dereva wa trela hilo aliingia barabarani bila kuwa mwangalifu na kumlazimu dereva wa basi moja la abiria kujaribu kumkwepa ,kabla ya basi hilo kukosa mwelekeo na kubingiria kwenye mto. Owino alisema waliouawa wakati basi hilo lilipobingiria kwenye mto Siyapei ni pamoja na wanaume sita,wanawake wanane na watoto watatu.Basi hilo lilikuwa safarini kutoka Kendu bay hadi hapa Nairobi kupitia barabara ya Narok.Takwimu zimeonyeshaa kuwa takriban watu elf tatu hufariki kila mwaka kwenye barabara za humu nchini ,lakini shirika la afya duniani WHO limesema idadi hiyo huenda iko juu zaidi.