Ngengi azuiliwa na Idara ya upelelezi kufuatia ajali ya hivi maajuzi

Idara ya upelelezi imesema inamzuilia Denis Muigai Ngengi , baada ya kujitokeza kama shahidi kwenye ajali mbili zilizotokea hivi majuzi katika kaunti za Muranga na Nakuru.Taarifa iliyotiwa siani na msajili mkuu wa idara hiyo P. Ndunda, alisema uchunguzi umebainisha kwamba mshukiwa huyo amewahi kushtakiwa kwa makosa manane awali A�yakiwemo ya wizi , kutoa habari za uongo,kujeruhi, uharibifu wa mali kimaksudi na kusingizia akitumia majina tofauti.Ndunda amesema matokeo ya kesi hizo nane hayajatolewa lakini habari zimesambazwa katika vituo vya Polisi vilivyoshughulikia kesi hizo ambako kumbukumbu zilizoko kumhusu ziko katika majina tofauti. Aliongeza kusema kwamba majina ya sasa anayotumia ambayo ni Denis Muigai Ngengi, ndiyo aliyojipa hivi majuzi. Ngengi alidai kwamba alishuhudia ile ajali mbaya ya barabarani ya Jumatatu iliyopita iliyomhusu gavana wa kaunti ya Nyeri marehemu A�Wahome Gakuru huko Kabati,kwenye barabara kuu ya Muranga��a- Thika.Pia alidai kushuhudia ile ajali ya ndege aina ya Helikopta iliyoanguka majuma matatu yaliyopita katika ziwa Nakuru na kuwaua watu watano waliokuwa wameabiri helikopta hiyo.

A�