Democrasi ya Kongo yakumbwa na baa kubwa la njaa

 

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inakumbwa na janga kubwa huku mamilioni ya watu wakikabiliwa na baa la njaa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema A�takriban watu milioni 13.1 wanahitaji kwa dharura msaada wa chakula. Hali hiyo inazidishwa na ongezeko la wakimbizi wanaotoroka ghasia nchini Kongo ambao kufikia sasa wamefikia milioni 4.4. Baraza hilo linasema ipo haja ya kushughulikia suala la makundi ya wanamgambo katika Jamhuri hiyo pamoja na kuandaa uchaguzi huru na wa haki. Uchaguzi mkuu nchini humo umepangiwa kufanyika tarehe 23 mwezi Disemba mwaka huu lakini haijabainika ikiwa rais Joseph Kabila atajiondoa.