Demockasia ya Kongo kuwa na uchaguzi mwishoni mwa mwezi disemba mwaka huu

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Bruno Tshibala amethibitisha kuwa uchaguzi wa urais utaandaliwa mwishoni mwa mwezi disemba mwaka huu. Hakikisho lake lilijiri huku tatizo la kibinadamu likikumba eneo la Kasai kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama. Hata hivyo, Bruno amesema hali hiyo imethibitiwa baada ya polisi na wanajeshi kupelekwa katika eneo hilo. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, maafisa wa usalama wamewaua raia kadhaa waliokuwa wakiandamana kulalamika kucheleweshwa kwa uchaguzi wa urais nchini humo. Kuna tetesi kuwa Jamhuri ya demokrasia ya Kongo huenda ikatumbukia katika lindi la ghasia za wenyewe kwa wenyewe.

A�