David Maraga asisitiza kushirikishwa kwa wanawake katika siasa za uchaguzi na uongozi

Jaji mkuu David Maraga amesema kuwa ushirikishi wa wanawake katika maswala ya kisheria na utekelezaji wa haki ni muhimu katika kuafikia taasisi thabiti, zenye amani na zinazotekeleza haki. Kulingana na Maraga, maonevu ya kijinsia katika utekelezaji wa haki aidha kutokana na sababu za kitamaduni ama sheria za ukandamizajiA� ni kikwazo kikubwa katika kuafikia malengo ya maendeleo. Akiongea wakati wa kongamano la kanda la chama cha kimataifa cha majaji wanawake katika hoteli moja jijini Nairobi, jaji mkuu pia alisisitiza haja ya kuimarisha ushirikishi wa wanawake katika siasa za uchaguzi na uongozi kwa ujumla . Alisema kuwa hii inaweza kuafikiwa kupitia kuondolewa kwa vikwazo vya kitamaduni wanavyokumbana navyo wanawake ikiwa ni pamoja na dhulma dhidi yao hasa wanazokumbana nazo wanawake wanaojiingiza katika masuala ya kisiasa.Jaji mkuu huyo aligusia masuala ya utekelezaji wa uwakilishi sawa wa kijinsia wa thuluthi mbili na kuonekana kupinga wale wasiopendelea hali hii akisemaA� itakuwa silaha kwa wale wanaonufaika kuendeleza ukandamizaji wa haki ama maonevu hasa kuhusiana na uafikiaji wa haki za kiuchumi na kijamii.