Cyril Ramaphosa kumrithi rais Jacob Zuma

Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC kimemchagua Cyril Ramaphosa kumrithi rais Jacob Zuma kama kiongozi wa chama hicho kikongwe.Aliyekuwa naibu wa rais na waziri na mke wa Zuma,Nkosazana Dlamini Zuma alishindwa kwenye mchakato wa uchaguzi huo.Ramaphosa sasa yuko katika nafasi nzuri ya kuwa rais wa Afrika kusini wakati wa uchaguzi wa urais mwaka 2019.Kinyanga��anyiro cha uongozi wa chama hicho kilifikia kileleta huku mgawanyiko ukionekana bayana kwenye uongozi wake.Hatimaye Ramaphosa alimshinda mpinzani wake Dlamini-Zuma kwa kura 2,261 kwa kura 2,440.Matokeo hayo yalisababisha shangwe ,vifijo na nderemo kwenye barabara za jiji kuu la Afrika kuini ,Johanesburg.Iliarifiwa kuwa matokeio ya kura hiyo yalicheleweshwa baada ya kambi ya Dlamini-Zuma kutaka shughuli ya kuzihesabu irudiwe.Upigaji kura ulimalizika siku ya jumapili.