Cyril Ramaphosa atangaza baraza lake la mawaziri

Rais mpya wa Afrika KusiniA�A�Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake la mawaziri na kufanya mabadiliko katika nyadhifa hizo za uwaziri . Alimteuwa tena Nhlanhla Nene kuwa waziri wa fedha na kubatilisha kufutwa kwake kazi na aliyekuwa rais Jacob Zuma. Zuma, anayekabiliwa na mashtaka ya ufisadi, alilazimishwa kujiuzulu mapema mwezi huu na chama chake . RamaphosaA�A�aliahidi kuleta mwamko mpya katika nchi hiyo na kukabiliana vilivyo na ufisadi.

Akitangaza uteuzi huo huko Pretoria , alisema kuwa katika kufanya mabadiliko hayo, alitilia maanani haja ya kuwa na uthabiti na maendeleo ya kiuchumi kwa ufufuzi wa uchumi na mabadiliko ya haraka.