Cyril Ramaphosa aonya kuhusu unyakuzi wa ardhi

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameonya kuhusu unyakuzi wa ardhi huku chama tawala cha ANC kinapoanza kufanya marekebisho ya sheria kuhusu  kukombolewa kwa  mashamba bila ulipiaji wa ridhaa.

Swala la ardhi limesalia kuwa tete nchini Afrika kusini,huku sehemu kubwa ya ardhi ikiwa ingali inashikililiwa  na wazungu wachache,miongo miwili baada ya kutanguliwa kwa utawala wa kibaguzi.Japo serikali ya ANC iliahidi kushughulikia swala hilo,bado sehemu kubwa ya mashamba ingali inamilikiwa na wazungu.Mapema wiki hii hatua ya serikali kuyatwaa mashamba yasio na wamilikaji viungani mwa majiji ya Johanesburg na  Pretoria ilizuia makabiliano makali na polisi na wamiliki wa mashamba makubwa.