Cynthia Onyango ashinda tuzo ya Startimes/SJAK

Mlinda lango wa timu ya mchezo wa magongo ya akina dada ya Telkom Kenya Cynthia Onyango ndiye mshindi wa tuzo ya Startimes/ SJAK ya mchezaji bora wa mwezi wa Januari. Onyango aliwapiku wachezaji tenisi Ryan Randiek na Sneha Kotecha na bondia Nick Okoth. A�Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka shirini na minne alichaguliwa na jopo la wanahabari baada ya kuibuka mlindalango bora kwenye mashindano ya kuwania taji ya klabu bingwa barani Afrika nchini Ghana mwezi uliopita. Onyango alifungwa mabao mawili katika mechi sita huku Telkom, ambao ni washindi mara tisa katika mashindano hayo wakichukua nishani ya fedha baada ya kushindwa bao moja sufuri na timu ya halimashauri ya ukusanyaji ushuru ya Ghana kwenye fainali na kujishindia tuzo ya mlinda lango bora kwenye mashindano hayo. Mlinda lango huyo anayechezea A�timu ya taifa alituzwa televisheni ya A�inchi arubaini na mbili na A�shilingi laki moja. Washindi wa awali A�wa tuzo hiyo wanajumuisha A�mwanariadha asiye na uwezo wa kusikia Simon Kibai A�Cherono, mwanariaha Helen Obiri, Janet Okelo wa mchezo wa raga, Ismail Changawa wa Tenisi A�na bondia Fatuma Zarika A�miononi mwa wengine wengi.