Cristiano Ronaldo ndiye wakwanza kufunga bao barani Ulaya

Kimataifa, mshambulizi wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika kila mchuano wa makundi wa ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya, huku mabingwa hao wakiishinda Borussia Dortmund mabao 3-2 jana usiku uwanjani Santiago Bernabeu.
Ronaldo alifunga bao lake la tisa kwenye ligi hiyo msimu huu kutoka nje ya mstatili. Kufikia sasa, mchezaji huyo amefunga jumla ya mabao 114 kwenye ligi hiyo ya bara Ulaya, mabao 17 zaidi ya mshambulizi wa Baselona, Lionel Messi. Timu hiyo inayofunzwa na Zinedine Zidane, huenda ikachuana na Roma, Besiktas, Paris St-Germain, Manchester City, Manchester United au Liverpool, kwenye raundi ya timu 16 bora ambayo droo yake itafanywa Jumatatu wiki ijayo.