COTU yawaonya magavana kuwafuta wafanyakazi wa kaunti kwasababu za kisiasa

Muungano wa vyama vya wafanyikazi hapa nchini-COTU umeelezea wasiwasi wake kuhusu hatua ya baadhi ya magavana hapa nchini ya kuwafuta kazi wafanyikazi kwasababu ya miegemeo yao ya kisiasa. Kwenye taarifa, muungano wa COTU umewaonya magavana dhidi ya kuchukua hatua za aina hiyo, ukisema utatumia taratibu za kisheria kuhakikisha haki inatendeka kwa wafanyikazi watakaoathiriwa. Baadhi ya magavana walioapishwa wamewapa likizo ya lazima baadhi ya maafisa waliopata afisini, katika kile kinachoonekana kuwa kukabili wapinzani. A�Tayari baadhi ya magavana wamewasimamisha kazi wafanyikazi wa serikali za kaunti kwa sababu zinazoonekana kuwa za kisiasa.A� Baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa ni kaunti za Siaya, Taita Taveta, Meru, Kiambu na Migori.