COTU Yaongeza Ada Inayotozwa Wafanyikazi

Wafanyikazi walio katika vyama vya wafanyikazi sasa watagharimika zaidi baada ya muungano wa vyama vya wafanyikazi hapa nchini-COTU kuamua kuongeza mchango wao wa kila mwezi kwa shilingi 50 kuanzia mwezi ujao. A�Kulingana na COTU, ada hiyo mpya itawezesha muungano huo kuendesha shughuli zake kwani kiwango cha sasa hakitoshi. Katibu mkuu wa muungano huo, Francis Atwoli, amesema wamekuwa wakitatizika kufadhili baadhi ya shughuli zao, ikiwa ni pamoja na kulipa mawakili wanaowakilisha wafanyikazi pamoja na kufungua taasisi za kuwafunza maafisa wa maswala ya leba. Nyongeza hiyo iliafikiwa baada ya mkutano wa kiushauri baina ya vyama vya muungano huo mapema mwaka huu. Nyongeza hiyo inatarajiwa kuwa mzigo kwa baadhi ya wafanyikazi ambao wamelipa ada ya shilingi-100 kwa kipindi cha miaka-7 iliyopita