Watu 286,122 wafariki dunia kutokana na makali ya Covid-19 duniani

Chamko la Covid-19 limesababisha vifo vya takriban watu 286,122 kote duniani tangu kuzuka kwake nchini China mwezi Disemba mwaka 2019.

Habari hizo ni kulingana na takwimu zilizokusanywa na shirika la habari la AFP.

Takriban visa 4,188, 040 vya maambukizi ya covid-19 vimeripotiwa katika mataifa 195.

Hata hivyo wahasiriwa 1, 432, 700 wamepona maambukizi hayo kote duniani.

Takwimu hizo zilizokusanywa na shirika hilo la AFP kutoka mataifa mbali mbali na shirika la afya duniani, ni kiasi kidogo cha idadi kamili ya  maambukizi ya Covid-19.

Amerika inaongoza kwa idadi ya vifo vilivyotokana na virusi vya korona huku watu 80,684 wakiwa wamefariki nchini humo.

Uingereza inafuata kwa karibu ikiwa imeripoti vifo 32,065 kutokana na maambukizi 223, 060.