CORD Kupanga Maandamano Mwezi Januari

Muungano wa CORD umetoa wito wa kufanyika kwa maandamano kuanzia tarehe 4 mwezi Januari mwaka ujao kulalamikia kupitishwa bungeni marekebisho sita za sheria ya uchaguzi. Wakiwahutubia wanahabari jijini Nairobi, vinara wa muungano huo Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetanga��ula waliishtumu Jubilee kwa kujaribu kutatiza utekelezaji haki. Hata hivyo walisema maandamano hayo yatakuwa ya amani. Wapinzani walisema kuwa marekebisho kwenye sheria ya uchaguzi ni kinyume cha sheria kwani sheria zinazorekebishwa zilipitishwa baada ya mashauriano. Vinara hao walisema kuwa wapinzani wataendeleza juhudi zao hadi pale marekebisho hayo yatakapobatilishwa.
Mnamo mwezi Mei mwaka huu wapinzani hao waliitisha maandamano ya barabarani kuwaondoa afisini makamishna wa IEBC ambayo baadaye yalizua ghasia zilizosababisha vifo vya baadhi ya waandamanaji kwenye baadhi ya ngome za wapinzani