Constantino Chiwenga atoa wito kwa wanazimbabwe kudumisha utangamano na utulivu

Jenerali mkuu wa kijeshi nchini Zimbabwe Constantino Chiwenga ametoa wito wa kudumisha kwa sheria na utangamano baada ya hatua ya kujiuzulu kwa rais Robert Mugabe kusababisha sherehe na kuliweka taifa hilo katika hali isiyojulikana. Akiwatubia wanahabari, jenerali huyo alitoa wito kwa raia wote wa taifa hilo kudumisha utulivu. Kujiuzulu kwa rais Robert Mugabe kulipokelewa kwa matumaini makubwa ya siku za usoni kwa raia wa taifa hilo kuambatana na maoni kutoka kwa jamii ya kimataifa. Uingereza ambayo ilikuwa mkoloni wa Zimbabwe ilipokea habari hizo kwa utayari wa kuisaidia Zimbabwe.