Chuo Kikuu Cha Masinde Muliro Chafungwa

Chuo kikuu cha Masinde Muliro kimefungwa kwa muda usiojulikana kufuatia ghasia za wanafunziA� waliokuwa wakipinga agizo la chuo hicho kwamba ili waweze kufanya mitihani wanapaswa kulipa karo yote bila ya kuwa na salio. Viongozi wa wanafunzi waliowahutubia wanahabari walisema kwamba wasimamizi wa chuo hicho waliwapa ilani na muda mfupi kumaliza karo yao kabla ya kufanya mitihani. Baraza la chuo hicho katika taarifa iliyotiwa saini na kaimu msajili wa maswala ya kimasomo na kuandikiwa wanafunzo waliogoma iliwaagiza wanafunzi hao kuondoka katika chuo hicho kabla ya saa tano asubuhi. Wanafunzi walilazimika kuharakisha kwenda nyumbani kufuatia agizo hilo. Polisi wa kupambana na ghasia waliitwa kutuliza ghasia na kuwatawanya waandamanaji ili kuepusha mali kuharibiwa na kurejesha utulivu.