Chuo Kikuu Cha Garissa Kufanya Ukumbusho Wa Shambulizi La Kigaidi

Maandalizi yamekamilika katika chuo kikuu cha Garissa huku chuo hicho kikijiandaa kwa hafla ya kumbukizi ya kwanza ya shambulizi la kigaidi la mwaka jana chuoni humo ambapo watu 148 waliuawa, wengi wao wanafunzi. Akiongea na wanahabari, mkuu wa chuo hicho Profesa Ahmed alisema shughuli nyingi zitatekelezwa wakati wa maadhimisho hayo. Miongoni mwa mambo yatakayotekelezwa ni pamoja na maombi ya madhehebu mbali mbali, mbio za umbali wa kilomita-5 ambazo zimeandaliwa kwa ukumbusho wa siku hiyo. Aidha profesa Warfa alisemaA�viongozi kadhaa akiwemo mbunge wa eneo hilo, Aden Duale wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo ambapo watatumbuizwa na makundi mbali mbali.A� Akikiri kwamba kisa hicho kilikuwa mojawapo wa matukio ya kusikitisha zaidi maishani mwake, Warfa alisema tukio la aina hiyo halipaswi kutokea mahali popote duniani. Alisema chuo hicho tayari kimefanikiwa kusajili wanafunzi 118 wa kibinafsi akiongeza kwamba shughuli ya kuwasajili wanafunzi 700 kwa mpango wa kawaida wa masomo itatekelezwa mwezi Septemba mwaka huu. Aliwahimiza wakenya wajitokeze kwa wingi siku ya Jumamosi kushirikiana na chuo hicho katika kuwakumbuka wenzao waliouawa kufuatia shambulizi hilo.