Chris Coleman ateuliwa kuwa kocha wa kilabu cha Sunderland

Chris Coleman ameteuliwa kuwa kocha wa kilabu cha Sunderland cha Uingereza baada ya kujiuzulu wadhifa wake katika timu ya taifa ya Wales. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 47 alitia saini mkataba wa miaka miwili unusu kuchukua nafasi ya Simon Grayson, aliyepigwa kalamu mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya kuongoza timu hiyo katika jumla ya mechi 18 pekee. A�Sunderland, iliyoshushwa ngazi katika ligi kuu Uingereza msimu uliopita inashikiia nafasi ya mwisho katika ligi ya daraja ya pili baada ya kushinda mechi moja tu kati ya 17 ambazo imecheza. Coleman kutoka Wales ni kocha wa 10 kuteuliwa tangu A�Roy Keane alipoondoka mwezi Disemba mwaka 2008.