China yazindua meli mpya ya kivita ili kuimarisha uwezo wake wa kijeshi

 

China imezindua meli mpya ya kivita ili kuimarisha uwezo wake wa kijeshi katika eneo hilo linalokumbwa na msukosuko. Meli hiyo ni pili ya kivita kuzinduliwa na China baada ya meli ya Liaoning. Vyombo vya habari nchini humo vilisema meli hiyo isiyokuwa na nahodha ilielekea baharini katika bandari ya Dalian iliyoko Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Habari za awali zilikuwa zimesema kuwa meli hiyo ya kivita ingelizinduliwa kwa shughuli za kijeshi mwaka-2020. Kumekuwa na majibizano makali kati ya Marekani na Korea Kaskazini katika siku za hivi punde. China ina meli moja tu ya kivita kwa jina Liaoning iliyonunuliwa kutoka Ukraine na kukarabatiwa. Marekani nayo imepeleka meli kadhaa za kivita na nyambizi katika eneo la Korea, jambo ambalo limezua ghadhabu kali kutoka kwa Korea Kaskazini. Meli hiyo ya China ina ndege za kivita aina ya Shenyang J-15 ingawa wadadisi wamesema uwezo wa meli hiyo hauwezi kufikia meli za kivita za Marekani.

A�