China yalaumiwa kwa kifo cha Liu Xiaobo mpizani mkuu wa serikali

China inakabiliwa na shutma za kimataifa kwa kuto-mruhusu mpinzani mkuu wa serikali, Liu Xiaobo, kupelekwa nga��ambo kwa matibabu. Mwana-harakati huyo aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 11 gerezani A�kwa tuhuma za uchochezi, alifariki hospotalini huko China akiwa na umri wa miaka 61. Miongoni mwa risala za kuomboleza kifo cha mwanaharakati huyo, kamati ya tuzo la Nobel, ambayo ilimtunukia tuzo la amani mwaka A�2010, imesema kwamba China inapaswa kubebeshwa dhamana kutokana na kifo chake. China sasa inahimizwa kumwachilia huru Mkewe, ambaye pia ni mtunzi wa mashairi Liu Xia, kutoka kifungo cha nyumbani. Ijapo China imejizuia kutoa taarifa yoyote rasmi, Gazeti moja linalomilikiwa na serikali A�limeshtumu watu fulani wenye ushawishi katika nchi za Magharibi kwa kuingiza siasa katika swala hilo. Liu alihamishwa kutoka gerezani hadi hospitali moja katika mji wa kaskazini-mashasriki wa Shenyang mwezi uliopita, ambako amekuwa akizuiliwa chini ya ulinzi mkali. Ujerumani ambayo ilifikiriwa kuwa mojawapo ya nchi ambako Liu angepelekwa, ilisikitika kufahamu kwamba jambo hilo halikutendeka kulingana na waziri wake wa mashauri ya nchi za kigeni Sigmar Gabriel.