Chiloba akanusha kuhusika katika wizi wa kura

Afisa mkuu wa tume ya IEBC Ezra Chiloba amekanusha madai ya mbunge wa Suna Mashariki, Junet Mohamed, kwamba anasaidia kufanikisha wizi wa kura kwa niaba ya chama tawala cha Jubilee kwenye marudio ya uchaguzi wa urais yaliyofanyika jana. Kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter jana jioni, Chiloba alisema kuwa madai hayo ya Junet yanaweza tu kuchochea taharuki zaidi nchini. Kwenye mkutano na wanahabari hapo jana Junet A�alisema kuwa Chiloba alienda likizoni baada ya kuhakikisha kwamba kuna mpango kabambe utakaomwezesha rais Uhuru Kenyatta kuchaguliwa tena. Mnamo Ijumaa iliyopita Chiloba alitangaza kwamba anachukua likizo ya majuma matatu ili kuwezesha kuandaliwa kwa uchaguzi wa jana. Chiloba alisema kuwa alifanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kwenda likizoni kufuatia shinikizo za upinzani ila hakutoa maelezo zaidi.