Chile Eboe-Osuji achaguliwa kuwa Rais wa mahakama kuu ya kimataifa ya ICC

Majaji wa mahakama ya kimataifa ya kushughulikia kesi za uhalifu wa kivita-ICC wamemchagua jaji Chile Eboe-Osuji wa Nigeria kuwa rais wa mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu. Jaji Robert Fremr kutoka jamhuri ya Czech alichaguliwa kuwa makamu wa kwanza wa rais wa mahakama hiyo huku jaji Marc Perrin de Brichambaut kutoka Ufaransa akichaguliwa kuwa makamu wa pili wa rais. Jaji Chile Eboe-Osuji alimshukuru mtangulizi wake, jaji Silvia FernA?ndez de Gurmendi pamoja na manaibu wake Joyce Aluoch na Kuniko Ozaki kwa uongozi wao busara. Asasi ya urais wa mahakama ya ICC inahusika na uratibu wa mpangilio wa shughuli za mahakama hiyo. Asasi hiyo pia hushirikisha shughuli za vitengo vingine na kushauriana na afisi ya kiongozi wa mashtaka kuhusu maswala ibuka.