Chelsea na Manchester City kuchunguzwa kuhusu usajili wa wachezaji chipukizi

Shirikisho la soka duniani FIFA, linachunguza vilabu vya Chelsea na Manchester City kuhusu usajili wa wachezaji chipukizi.A� Hii ni mara ya tatu shirikisho la FIFA kuchunguza kilabu cha Chelsea ambapo mwaka 2009 timu hiyo ilipigwa marufuku ya kuwasajili wachezaji kwa muda wa miaka miwili. Mwezi Mei, ligi kuu nchini Uingereza ilitoza kilabu cha Manchester City faini ya Pauni elfu mia tatu na kukipiga marufuku ya kuwasajili wachezaji kwa muda wa miaka miwili. Shirikisho la FIFA limeweka sheria kali kuhusu kusajiliwa kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 ili wasinyanyashwe au kuhamishiwa mataifa mengine kinyume cha sheria.