Chebukati ataka makamishina waliojiuzulu kubani malengo yao

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka, Wafula Chebukati amewataka ma-kamishna wawili waliorejea kazini baada ya kujiuzulu mwezi April wamwandikie barua za kubaini malengo yao.

Tume hiyo ina upungufu wa makamishna wane kufuatia kung’atuka kwa naibu wa mweneykiti Connie Maina, na pia makamishna Margaret Mwachanya, Paul Kurgat, na Roselyne Akombe.

Maina na Mwachanya walirejea katika ofisi zao kufuatia uamuzi wa mahakama tarehe 10 Augosti kwamba hawakufuata utaratibu ufaao wakati wa kuondoka kwao. Chebukati aliwaambia wana-habari  hii leo kwamba baada ya makamishna hao kumwandikia barua, tume ya (IEBC) itashughulikia maswala yote watakayokuwa wameibua.

Awali, Chebukati alidumisha kwamba Ma-kamishna hao watatu; wawili ambao walirejea ofisini siku ya Ijumaa walijiuzulu nyadhifa zao. Chebukati alisema kwamba wawili hao hawawezi wakakubaliwa kurejea ofisini baada ya kusalimisha mali zote za tume hiyo  sawia na taratibu nyingine za kuondoka ofisini.