Charity Ngilu ameanzisha upya uchimbaji wa mkaa wa mawe

Serikali ya kaunti ya Kitui imeanzisha upya mikakati ya kuzindua uchimbaji makaa ya mawe kwenye bonde la Mui. Gavana mpya wa kaunti ya Kitui, Charity Kaluki Ngilu amesema uchimbaji makaa ya mawe ni njia moja ya kuimariasha maisha ya wakazi wa kaunti hiyo ambayo hushuhudia ukame wa mara kwa mara. Hata hivyo wakazi wanahofia kuwa kuanzishwa kwa miradi hiyo katika maeneo ya Mui na Ngaaie huenda kukasababisha kufurushwa kwao kutoa nafasi ya uchimbaji huo. Aidha wanaharakati wa mazingira wanapinga matumizi ya makaa ya mawe yanayokisiwa kuchafua mazingira. Makaa ya mawe hutoa gesi ya carbon dioxide inayokisiwa kuharibu utandu wa ozone.