Changamoto Ya Jammeh Kuhusu Uchaguzi Yaahirishwa

Mahakama ya juu  kabisa nchini Gambia imesema haina uwezo wa kusikiza rufaa inayotaka  kubanduliwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi  jana hadi mwezi wa Mei ambapo majaji waliokuwa wakitarajiwa  kuisaidia mahakama hiyo kutoa uamuzi hawakufika.Jaji mkuu Emmanuel Fagbenle aliahirisha kutoa umamuzi wa kesi hiyo hadio tarehe 16 mwezi huu.Hii inamaanisha kuwa mahakama hiyo itasikiliza rufaa ya chama cha  rais Yahya Jammeh cha APRC,siku mbili tu kabla ya kumalizika rasmi kwa kipindi chake cha utawala.Jaji Fagnbele  alisema angependa taifa hilo lijitatulie mizozo yake ya kisiasa kupitia juhudi za viongozi wa jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi-ECOWAS.Viongozi hao watajaribu kumshawishi aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jamme kukubali kukabidhi mamlaka kwa  mpinzani wake ambaye alishinda uchaguzi huo Adama Barrow.Miongoni mwa viongozi wa ECOWAS watakaoshughulikia swala hilo ni kiongozi wa Nigeria Muhamadu Buhari