Chama Kipya Cha Jubilee Chazinduliwa

Chama kipya chaA� Jubilee PartyA� kitazunduliwa rasmi katika kipindi cha mwezi mmoja ujao. RaisA� Uhuru Kenyatta akiandamana na naibu Rais William Ruto walitangaza hayo katika ikulu ya Nairobi wakiwa na viongozi wa vyama 12 vya kisiasa ambavyo vimetangaza kuwa vitavunjiliwa mbali na kujiunga na chama hicho kipya cha Jubilee. Rais Kenyatta alisema vyama vyote tanzu vya Jubilee vitaanda mikutano yao ya kitaifa ya wajumbe tarehe nane mwezi Septemba kuratibu hatua ya kuvivunjilia mbali kabla ya kujiunga na chama kipya cha Jubilee. Rais Kenyatta alisema kuwa chama hicho kipya kutatatua tatizo la siasa za kijamii pamoja na kudumisha umoja nchini.

Kiongozi wa taifa pia aliwahakikishia walio na azima ya kuwania nyadhifa za uchaguzi kwaA� tikiti ya chama cha Jubilee kwamba hakuwakuwa na mapendeleo yoyote wakati wa shughuli ya kuwateua wagombeaja wa chama hicho ambayo itaendeshwa kwa njia ya kidemokrasia. Alisema shughuli hiyo ya uteuzi itasimamiwa na tume huru ya uchaguzi kuhaikisha kwamba demokrasia inadumishwa na hakuna mapendeleo.