Chama cha Wiper kukutana kuratibu mikakati ya kinyanga��anyiro cha urais 2022

Chama cha Wiper kitakutana leo kuratibu mikakati yake kabla ya kinyanga��acha nyiro cha urais mwaka 2022. Kwenye taarifa, chama hicho kimesema kauli mbiu ya mkutano huo ni kushinikiza kiongozi wa chama hicho Kalonzo Musyoka kuwa mgombeaji urais wa mrengo wa upinzani. Pia hatua ya Musyoka ya kutohudhuria uapisho wa Raila itaangaziwa. Mkutano huo unajiri huku uvumi ukizagaa kuwa hatua ya Musyoka, Musalia Mudavadi wa chama cha ANC na Moses Wetangula wa chama cha Ford Kenya ya kuto-hudhuria hafla hiyo ni ishara ya kujitenga na Raila Odinga kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.