Chama cha wauguzi chaapa kuendelea na mgomo

Chama cha kitaifa cha wauguzi kinasisitiza kwamba hakitasitisha mgomo unaoendelea wa wauguzi hadi serikali itakapotia saini makubaliano nao. Akiongea na wanahabari katika bustani ya uhuru Park, Katibu mkuu wa chama hicho Maurice Opetu alisema serikali inajikokota katika kushughulikia mzozo huoA� na akasema chama hicho kinaendelea kutetea maslahi ya wauguzi ili kuhakikisha wanalipwa vyema. Alikanusha madai ya magava kwamba wamejiondoa kwenye mashauri na magavana.

Wauguzi hao sasa wanatoa wit kwa wizara ya lebaA� iingilie kati na kusuluhisha mzozo huo ili waweze kurejea kazini.