Chama Cha Walimu KUPPET Tawi La Meru Chaagiza Kikao Na TSC

Maafisa wa chama cha KUPPET katika kaunti ya Meru wameitaka tume ya kuajiri walimu kushauriana na chama hicho kuhusu utekelezaji wa kandarasi za utendakazi kwa walimu. Katibu wa tawi la Meru la chama cha KUPPET, Karuti Nchebere amesema walimu wanaunga mkono kandarasi hizo za utendakazi lakini maslahi ya walimu sharti yatiliwe maanani. Nchebere alisema Kenya inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu, jambo ambalo limeathiri ubora wa elimu. Nchebere alisema walimu wengi wamekosa motisha kwasababu ya kutolipwa marupurupu ya kufanya kazi ya ziada. Alisema walimu hawana raha hasa kutokana na kutibuka kwa pendekezo la kuwaongeza mshahara mwaka uliopita.