Chama cha ODM Chafadhaishwa na Kuondolewa Kwa Walinzi wa Magavana

Chama cha ODM kimefadhaishwa na hatua ya kuondolewa kwa baadhi ya walinzi wa magavana Ali Hassan Joho na Amason Kingi wa Mombasa naA� Kilifi mtawalia.

Chama hicho kinamtaka rais Uhuru Kenyatta na waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery kuagiga kurejeshwa kwa walinzi hao mara moja.

Akihutubia wanahabari hapo jana, gavana wa Kakamega Wycliffe Opranya kwa niaba ya kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga alisema hatua hiyo ni ukiukaji wa katiba na kwamba inarudisha nyuma taifa hili.

Oparanya alisema upinzani nchini utailazimisha serikali kuwajibikia lolote ambalo huenda likawapata magavana hao ambao walihusika kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Malindi ambapo Willy Mtengo wa chama cha ODM aliibuka mshindi.

Wakati huo huo Oparanya aliitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka kumchukulia hatua waziri wa kawi Charles Keter kwa kujihusisha na kampeni za uchaguzi mdogo wa useneta katika kaunti ya Kericho ambapo alidaiwa kutumia mali ya umma.