Mahakama Yaongeza siku tatu za usajili wa wapiga kura

Mahakama kuu imeongeza muda wa zoezi kubwa la usajili wa wapiga kura kwa siku tatu hadi siku ya Jumapili tarehe 19 Februari mwaka huu wa 2017. Awali, Jaji wa mahakama hiyo Chacha Mwita alikuwa ameongeza muda huo kwa siku mbili ambao ungemalizika jana. Uamuzi wa jana wa Jaji Mwita ilitolewa kwenye kesi iliyiowasilishwa na mwana-harakati Okiya Omtatah, ambaye alitaka zoezi hilo kuendelea hadi kusalia miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Augosti. Omtatah alikuwa ameibua maswala mengine kadha, ambayo sasa yatashughulikiwa na mahakama kuanzia tarehe 2 mwezi marchi. Miongoni mwa matakwa ya mwana-harakati huyo ni kwamba mahakama kuilazimisha tume huru ya uchaguzi na utaribu wa mipaka nchiniA� (IEBC), kusajili wapiga kura kwa kutumia cheti za kuzaliwa na pia passporti ambazo muda wake wa matumizi umemalizika kwani wapiga kura wengi wameshindwa kujisajili kwa vile hawana vitambulisho. Hata hivyo, kipindi cha ziada cha siku mbili za usaji wa wapiga kura kimeshuhudia idadi ndogo ya wanaojitokeza kwa zoezi hilo. Wakati huo huo; zoezi la kusajili wakenya wanaoishi ugenini kuwa waopiga kura litafanyika tareheA� 20 FebruariA� hadi tarehe 3 mwezi Marchi.