Cecil Kariuki kuzungumza na wanahabari kabla ya sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa kuhusu malaria

Waziri wa afya Cecil Kariuki anatarajiwa leo kuzungumza na wanahabari kabla ya sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa kuhusu malaria tarehe 25 mwezi huu. Siku hii huadhimishwa kote dunianiA� na humulika harakati za kimataifa ambazoA� zimechukuliwa kupambana na ugonjwa huo hatari na wakati huo huo kutambua naA� kujivunia maendeleo ambayo yamepigwa katika Nyanja hiyo.

Tangu waka wa 2000,maendeleo makubwa yamepatikana katikaA� ukabilianaji na ugonjwa wa malaria na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu. Hata hivyo nusu ya idadi ya watu duniani ,bado inakabiliwa na hatari ya ugonjwa huo ambao unaweza kuzuiwa na hata kutibika.MalariaA� huangamiza maisha ya mtoto mmoja, kila dakika mbili duniani.