Cech Atuzwa Taji La Mchezaji Bora Czech Republic

Mlindalango wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech, Petr Cech wa Asenali alitajwa mchezaji bora wa mwaka nchini humo kwa mara ya nane jana usiku kwenye kura zilizopigwa na makocha, wachezaji na maafisa wa vilabu nchini humo. Cech mwenye umri wa miaka 33, ameichezea nchi yake jumla ya mechiA�A� 118 tangu aliposhiriki katika mechi za kimataifa kwa mara ya kwanza mwaka 2002 na aliwapiku wenzake David Lafata ambaye ni mshambulizi wa timu ya Sparta Prague, na kiungo wa timu ya Hertha Berlin, Vladimir Darida. Cech alijiunga na Asenali kutoka timu ya Chelsea ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza mwezi Juni baada ya kuichezea Chelsea jumla ya mechi 400 katika kipindi cha miaka 11.