Carol Wanjiru Karugu ateuliwa kuwa naibu wa gavana Nyeri

 

Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga amemteuwa Carol Wanjiru Karugu kuwa naibu wake.Wanjiru atakuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu kwenye wadhifa wa naibu wa gavana.Jina lake liliwasiishwa katika bunge la kaunti hiyo siku ya alhamisi alasiri ili kuidhinishwa.

 

Hadi wakati wa uteuzi wake Carol alikuwa afisa mkuu wa kampuni ya Jabali Microserve Ltd,kampuni ya kibiashara ambayo ni sehemu ya Wakfu wa Jitegemee ambayo hujishuhgulisha na uwekezaji wa kijamii.Ana tajriba ya takribanA� miaka 15 katika maswala ya masoko ya hisa ya kikanda na sekta ya huduma za kifedha.Kiti hicho kiliwachwa wazi wakati ambapo Kahiga alipandishwa cheo na kuwa Gavana kufwatia kifo cha aliyekuwa gavana wa tatu wa kaunti hiyo Wahome Gakuru katika ajali ya barabarani mwezi wa Novemba mwaka jana.