Magavana wakutana kuwachagua maafisa wapya

Magavana kutoka kaunti zote 47 wanakutana leo katika hoteli moja jijini Nairobi kuwachagua maafisa wapya kuambatana na sheria kuhusu baraza la magavana.Wakati wa mkutano huo, mwenyekiti wa sasa Peter Munya hatatetea wadhifa huo baada ya kuhudumu kwa miaka miwili.Munya hata hivyo anatarajiwa kutoa hotuba kuhusu hali ya ugatuzi hapa nchini.Munya ni mwenyekiti wa pili wa baraza hilo baada ya gavana wa Bomet Isaac Ruto.Mwenyekiti mpya atakayechaguliwa wakati wa mkutano huo atahudumu kwa miezi miwili pekee ikiwa haitachaguliwa tena kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.