Bweni Lateketezwa Katika Shule Ya Upili Ya Aiyebo Huko Baringo

Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa iliharibiwa wakati moto ulipoteketeza bweni katika shule ya upili ya wavulana ya Aiyebo huko Baringo kaskazini. Mwalimu mkuu wa shule hiyo Stanley Amdany amesema kuwa hakuna aliyejeruhiwa katika mkasa huo ambao ulitokea wanafunzi wakiwa darasani. Mkurugenzi wa elimu katika eneo la Baringo kaskazini Wilson Korombori alisikitikia kisa hicho na kusema kuwa wadau watakutana ili kutafuta namna ya kushughulikia hasara iliyopatikana.