Bunge nchini Uganda lachukuwa hatua kufutilia mbali kigezo cha umri wa urais

Bunge nchini Uganda limechukuwa hatua za kwanza katika kufutilia mbali kigezo cha umri wa urais ambao utamwezesha rais wa sasa Yoweri Museveni kusalia mamlakani. Ghadhabu ilitanda kwa siku ya pili hapo jana kuhusiana na mpango unaoungwa mkono na wabunge wa chama cha National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na Museveni wakiwasilisha mswada wa kufutilia mbali umri wa urais na kumruhusu rais huyo wa umri wa miaka 73 kuwania urais kwa kipindi cha sita mnamo mwakaA� 2021. Wabunge walivunja vipaza sauti na kukabiliana kwa ngumi na kurushiana viti huku maafisa wa usalama wakijaribu kuwaondoa wabunge 25 waliozuiwa na spikaA� wa bunge Rebecca Kadaga kuhudhuria kikao cha bunge baada ya kuhusika katika malumbano kama hayo siku iliyopita . Licha ya mtafaruku huo, mswada huo uliowasilishwa na mbungeA� Raphael Magyezi ulipitishwa na wabunge wanaoiunga mkono serikali baada ya kiongozi wa upande wa upinzani bungeni , Winnie Kiiza wa chama chaA� Forum for Democratic Change (FDC), kuongoza wabunge wake nje ya bungeA� . Wanaounga mkono mswada huo walisema kuwa kigezo cha umri huwabagua wazee.