Bunge lapunguza muda wa kuchapisha mswada wa kurekebisha sheria za uchaguzi

Bunge jana lilipiga kura kupunguza muda wa uchapishaji mswada wa kurekebisha sheria za uchaguzi kutoka siku 14 hadi siku moja. Hii inamaanisha kwamba kamati ya bunge sasa inaweza kualika umma mara moja kutoa maoni kuhusu mswada huo kuanzia leo kabla ya ripoti kuwasilishwa bungeni. Kupunguzwa kwa muda wa uchapishaji mswada huo pia kunamaanisha kwamba mswada huo utachukua muda mfupi zaidi bungeni kabla ya kupitishwa na kuidhinishwa na rais kuwa sheria. Wabunge wa muungano wa NASA waliokuwepo bungeni walipinga hoja hiyo lakini walishindwa kwa wingi wa kura 144 ya wabunge waliounga mkono hoja hiyo dhidi ya kura 53 za wabunge waliopinga hoja hiyo. Kwenye mswada huo, chama cha Jubilee kinanuia kuwaruhusu makamishna wa tume ya IEBC kumchagua miongioni mwao mwanachama atakayetangaza matokeo ya uchaguzi wa urais iwapo mwenyekiti wa tume hiyo au naibu mwenyekiti hawako. Mswada huo pia unalenga kufanya utumiaji wa mfumo usio wa kielektroniki wa kuwasilisha matokeo ya uchaguzi kuwa lazimaA� na iwapo kutakuwa na utata kwenyeA� matokeo yaliyowasilishwa kwa njia ya kielektroniki basi yale yaliyowasilishwaA� kwa njia isiyo ya kielektroniki yatatumika. Vile vile mswada huo unalenga kujumuisha kwenye sheria kuwa iwapo mgombeaji atajiondoa kwenye marudio ya uchaguzi, mgombeaji aliyesalia atatatangazwa kuwa amechaguliwa moja kwa moja kuwa rais. Afisa yeyote msimamizi wa uchaguzi atakayekataa kutia saini stakabadhi zote za uchaguzi atahukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani iwapo mswada wa marekebisho ya sheria kuhusu hatia za kiuchaguzi utapitishwa.