Bunge Lapitisha Mwada Wa Marekebisho Ya Sheria Kuhusu Benki 2015

Bunge la taifa limepitisha mswada wa marekebisho ya sheria kuhusu benki wa mwaka 2015,ambao ukitiwa saini kuwa sheria , benki za biashara zitatoza riba ya asilimia 4 ya kiwango cha benki kuu.Rais Uhuru Kenyatta akitia saini mswada huo,benki za biashara zitahitajika kutoza kiwango cha riba kisichozidi asilimia 14.5.Mswada huo pia unapendekeza kwamba benki za biashara zilipe faida ya angalau asilimia 7 kwa akiba za wateja.Wabunge wametaja viwango hivyo vya juua vya riba kuwa chanzo cha bei ghali ya bidhaa msingi.Aidha wabunge walisema viwango vya juu riba vinawazuia Wakenya wengi kukopa pesa,ambazo wanahitaji kuanzisha au kupanua biashara zao ,ili kujiendeleza maishani.Benki za hapa nchini,chini ya chamaA� wamiliki wa benki zinatarajiwa kuandaa kikao hivi leo kuelezea hisia zake kuhusu hatua hiyo .